Michezo

Zolla D akimbiwa Ulingoni

1_Zola_akimbiwa_ulingoni

Mkali wa ngumi na muziki wa Hip Hop  katika mitindo ya Mix Fighter David Michael  Mlope, ama ukipenda unaweza kumwita King Zola D, hivi juzi amekimbiwa na mpinzani wake katika pambano lililoandaliwa na Kampuni ya Aulora, katika uwanja wa DDC mlimani Cyte.

 

Zolla amesema ingawa amepata ushindi wa Chee, lakini amehuzunika sana kwani amefanya mazoezi kwa muda mrefu akiwa na hamu ya kupigana, hatimaye mazoezi yote yamekuwa bule kwani mpizani wake ameingia mitini bila ya kuleta sababu za msingi.

 

Amesema huku ni kudumaa kwa ndundi kwa mtu kujitia woga usio wa msingi, kwani watu wametoa kiingilio kuja kuangalia ngumi sasa inakuwaje mtu ukimbie. Zola na Kiza kinene kama wangepigana ingekuwa ‘Game’ yao ya marudio kwani awamu ya kwanza walipigana mwishoni mwa mwaka 2009 kwenda 2010 na Kiza Kinene kupigwa vibaya na kuomba warudiane, lakini chaajabu leo hii wakati pambano limeshakamilika amekimbia wakati aliomba pambano kurudiana ni yeye.

Zola_D_Akiingia_na_Benja_mini
Zolla D akiwa na Benjamini wa mambo Jambo wakiingia kwenye ukumbi wa DDC

Zolla_akimsalimia_Ali_aurola

Zola D akisalimiana na Ali Aurola(Wa pili kutoka mkono wa kulia)

Zolla_akiwa_na_Aurola
Zolla D akiongea na simu, wakati akisubiri pambano

Zolla_akiwa_na_kocha_wake
Zola D akiwa na mmoja wa makocha wake, wakisubiri pambano

Zola_akiwa_na_Kerven_wakiwa_ulingoni
Zola Akiwa na Kerven akimsubiri mpizani wake, ajitokeze jambo ambalo halikufua dafu, kwani mwenzake mapemba akilikuwa akila bata nyumbani.

Zolaa_akiomba_asikimbiwe_ulingoni

Zola D akionyesha hisia zake kuudhunishwa kwa kutokuja kwa mpinzani wake.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents