Michezo

Zoezi la kupigia kura wasanii kwenye Kili Music Awards lazinduliwa rasmi

Zoezi la kupigia kura wasanii kwenye tuzo za Kili limezinduliwa leo ambapo kamati ya maandalizi leo imekutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea utoaji taarifa zinazohusisha mchakato wa kupata washindi katika kila kipengele.

IMG_0793

“Tarehe 2, mei 2013 ndio ilikuwa siku ya kwanza ya upigaji kura na zoezi linaonekana kwenda vizuri,” amesema meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe kwenye taarifa yake kwa waandishi wa habari.

“Mashabiki na wapenzi wa wasanii na kazi zao sasa muda ni wenu kuwapigia kura na kujitahidi kupunguza kukosea kwani kutamkosesha kura msanii wako,bendi yako ama kazi yako. Ili kupiga kura unatakiwa kuandika namba ya msanii,wimbo wako,kikundi au bendi unayoitaka na kisha kutuma kwenda namba 15345.”

IMG_0802

Meneja huyo wa bia ya Kilimanjaro ambao ni wadhamini wakuu wa tuzo hizo aliongea, “Njia nyingine zaidi ya ujumbe mfupi (SMS) ni pamoja na Email: Tuma email kwenda [email protected] au tembelea www.kilitimetz.com na upige kura moja kwa moja”

IMG_0797

Bwana Kavishe alimaliza kwa kuwakumbusha wapenzi wa muziki kuwa msimu wa tuzo hizo ni Desemba 2011 hadi Novemba 2012. “Msimu wa tuzo unamalizika mwezi Novemba ili kuzipa kazi nzuri za wasanii zinazotolewa mwezi Desemba kushindana kwa haki mwaka unaofuata ili kuepusha kuonekana ni mpya sana na ndo zinafanya vizuri katika chati mbalimbali”

Tuzo hizo zitatolewa June 8, katika ukumbi wa Mlimani City.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents