Zitto Kabwe kugombea urais mwaka 2015

Mara ya mwisho mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuweka wazi nia yake ya kugombea urais wa Tanzania ilikuwa kwenye kipindi cha Makutano cha Magic FM japo hakuweka wazi ni mwaka gani. Lakini jana kupitia Amplifaya ya Clouds FM, mbunge huyo kijana ameweka wazi mpango wa kutogombea tena ubunge bali atagombea cheo kikubwa kabisa nchini, urais mwaka 2015.

“Kwanza nawathibitishia nitagombea urais na hili liwe wazi kabisa kwenu wala halina mashaka niitagombea,kwahiyo kama kulikuwa kuna wasi wasi labda anasema tu ni siasa yaani hilo waliondoe,”alisema.

“Sitagombea tena ubunge kwasababu miaka 10 ambayo kama Mungu atakuwa amenifikisha 2015 salama, mambo ambayo nitakuwa nimeyafanya yale ambayo nitakuwa nitakuwa sijayafanya, ambayo nimeshindwa kuyafanya kwa miaka 10 sitaweza kufanya tena kama nitaongezewa miaka mingine 30 na huo ndiyo mwono wangu kiuongozi kwahiyo lazima niende next level na next level Tanzania ni urais kwahiyo kama wananchi wakiona aaaah!!!! bado bhana, bado mdogo au nini, mimi nitakubali kwasababu ndiyo huwezi kuwa lazimisha wananchi ‘lazima niwe kiongozi wenu’, wewe unawaambia nataka, lakini nataka kwasababu ajenda yangu ni hii, mimi sitaki urais kwasababu napenda kuwa rais, nataka kuwa rais kwasababu najua kuna kazi yakufanya ya kubadilisha hii nchi na kubadilisha mindset za watu Tanzania ambayo siiyoni kwa wanasiasa wengine.”

Aliongeza, “cheo ni njia ya kukufanya wewe uweze kukubaliana na changamoto ,changamoto za nchi, lakini ni lazima kabla ya kupata huo urais upitie chama, na mimi ni mwanachama wa CHADEMA toka na umri wa miaka 16.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents