Burudani

Zijengwe sober house za serikali kutasaidia waathirika wengi wa dawa za kulevya – Ray C

Msanii mkongwe wa muziki Ray C amefunguka kwa kusema kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii wanaounga mkono harakati za serikali za kupambana na biashara ya Madawa ya kulevya huku akiishauri serikali kujenga sober house ambazo zitawasaidia vijana ambao wameshaingia kwenye janga hilo.

Muimbaji huyo ambaye pia ni muathirika wa Madawa ya kulevya, amedai yeye alitumia nguvu kubwa mpaka kufanikiwa kuacha licha ya kushindwa mara kadhaa.

“Hili janga ulisikie tu kwa watu lakini lisikukute wewe,” Ray C alikiambia kipindi cha FNL cha EATV. “Ukiingia huku ndio utajua nini tunazungumza, ni mateso makubwa sana, unajiona upo kwenye giza nene, halafu kuna sauti unazisikia wewe ndio basi huwezi kutoka tena. Binafsi ningeishauri serikali ijenge sober haouse zake kuwasaidia vijana kwa sababu sober house nyingi ni zakulipia na watu hawana pesa,”

Aliongeza, “Nchi kama Kenya na Afrika Kusini wana sober zao ambazo zinawasaidia watu wengi sana, binafsi kwa kuwa nimepitia changamoto nyingi naona serikali ikifanya hivyo itasaidia watu wengi sana wa chini,”

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda hivi karibuni wakati akitangaza majina ya wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya alidai kwa tafiti ndogo aliyofanya amegundua tiba ya methadone ambayo imekuwa ikitolewa katika hospitali mbalimbali nchini haiwasaidii waathirika hao kwani baada ya kupungua idadi ya waathirika lakini wanaongezeka kila mwaka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents