Ziara ya Rihanna Malaysia utatani!

Mwanamuziki toka nchini marekani Rihanna anatarajiwa kuzuru nchini
Malaysia February 13. Katika nchi ambayo inatawaliwa kwa sheria za dini
ya Kiislam ni vigumu kuona onyesho la mwanamuziki kama Rihanna…

Mwanamuziki toka nchini marekani Rihanna anatarajiwa kuzuru nchini Malaysia February 13. Katika nchi ambayo inatawaliwa kwa sheria za dini ya Kiislam ni vigumu kuona onyesho la mwanamuziki kama Rihanna amabaye anakawaida ya kupagawisha mashabiki kwa mavazi yake ambayo yanarandana na umbo lake lenye mvuto kwa kila jicho.

 

Chama cha Pan-Malaysian Islamic Party kimekuwa cha kwanza kuipinga ziara ya mwanamuziki huyu nchini malaysia kwa madai kuwa haina manufaa kwa wamalay sana sana itaharibu culture ya wamalay.

 

Katika waraka wao PAS wanasema kuwa hawaungi mkono hata kidogo ziara ya mwanamuziki huyu na kutaka serikali kuivunjilia mbali ziara ya mwanamuziki huyu.

 

Ikumbukwe kuwa waandaaji wa The Pussycat Dolls waliishia kulipa fine ya Dola 3000 na kufungiwa kwa muda maalum kufanya shughuli za burudani baada ya kuchezesha wanamuziki nusu uchi hapa Malaysia.

 

Hivi karibuni PAS waliongoza mamia kwa maelfu ya waandamanaji kulaani mauaji ya Wapalestina huko Gaza, katika maandamano hayo ambayo yaliishia kwenye uwanja kubwa wa mpira wa Sha Alam, viongozi wa PAS waliwaasa wananchi wa Malaysia kugomea bidhaa za Marekani ikiwemo Coca Cola, Star Bugs, Mc Donald na nyinginezo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents