Burudani

Zari hawezi kuhamia Tanzania moja kwa moja – Diamond

Diamond Platnumz na Zari The Boss Lady tayari wameziunganisha familia zao kwa kumpata mtoto wao wa kwanza Tiffah, lakini hakuna mpango wa mrembo huyo Mganda kuhamia moja kwa moja Tanzania ili kutengezeza familia moja.

dai na zari

Diamond a.k.a Baba Tiffah licha ya kuwa amekuwa akitoa ahadi ya kufunga ndoa na Zari bila kusema lini, amesema kuwa hakuna mpango wa Zari kuhamia Tanzania moja kwa moja kutokana na kuwa na biashara zake Uganda na Afrika Kusini.

“Kusema Zari atakaa moja kwa moja kubase Dar, Tanzania itakuwa ni ngumu lakini atakuwa muda atakaokaa kule na huku ni sawa kabisa atakuwa Tanzania, atakuwa pia South Africa, atakuwa Uganda kwasababu anabiashara zake tofauti tofauti anazozifanya.” alisema Diamond alipokuwa akijibu swali la shabiki siku ya 40 ya Tiffah, aliyeuliza kama Zari atahamia Tanzania.

Aliendelea kusema;
“Sasa ukimwambia mtu abase na biashara zake kuzihamisha sio rahisi kihivyo…na huwezi kujua kibiashara itatengeza nini, na mwanzo wa mapenzi kufanya vitu vya kumkwamisha mwenzako kimaisha haiwezi kuleta maana.”

watoto wa zari

Tiffah ni mtoto wa nne kwa Zari, watoto wake watatu wa kiume aliowapata na mume wake wa zamani Ivan wanaishi Afrika Kusini yaliko makazi ya Zari. Huenda hiyo ikawa ni sababu nyingine japokuwa Diamond hakuitaja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents