Habari

Zanzibar Heroes na Kili Stars kuwapa raha Watanzania leo?

Timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) na timu ya taifa ya Tanzania bara (Kilimanjaro Stars) leo zinajitupa uwanjani kupambana na timu za taifa za Kenya na Uganda katika nusu fainali ya michezo ya CecafaTusker Challenge Cup inayoendelea jijini Kampala.

Zanzibar Heroes ndiyo itakuwa ya kwanza kushuka dimbani na kupambana na Kenya majira ya saa nane mchana wakati Kilimanjaro Stars itaingia uwanjani majira ya jioni kupambana na wenyeji Uganda katika mtanange unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents