Habari

Zanzibar Career Fair Event (Nov 22), vijana kufundishwa kutengeneza CV, kujiandaa na usaili wa kazi

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa kushirikiana na kampuni ya VSO Tanzania na Shell Company kwa pamoja wameandaa tamasha la Zanzibar Career Fair Event siku ya tarehe 22/11/2014 ndani ya Ukumbi wa Bwawani.

ZanziJobs_Flyer_SW (4)-page-0

Hiyo itakua nafasi kwa vijana kutoka vyuo mbali mbali Zanzibar kukutana uso kwa uso na makampuni mbali mbali yenye uwezo wa kuajiri. Tunatarajia kuwa na makampuni 30 katika Nyanja za ujenzi, uzalishaji pamoja na sekta ya utalii.

Jinsi ya kushiriki:

– Jiandikishe kupitia namba 0767578984 au tembelea ofisi za Wizara ya
Maendeleo ya Vijana Zanzibar ili uweze kujiandikisha.

– Kila mshiriki atapewa flash drive yenye mawasiliano ya makampuni mbalimbali.

– Mgeni rasmi atakua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Muheshimiwa Dkt. Ali Mohammed Shein

– Kutakuwa na CV clinic ambayo itawawezesha vijana kujifunza jinsi ya
kutengeneza CV na kujiandaa na usaili wa kazi.

Kumbuka nafasi ni chache hivyo jiandikishe mapema. Tembelea twitter: Zanzijobs na
Facebook Zanzijobs.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents