Yvonne Mwale: Alinyang’anywa urithi wote alioachiwa na wazazi wake


Kama umeshausikia na kuuona wimbo wa Fid Q, ‘Sihitaji Marafiki’ sura na sauti ya Yvonne Mwale si vigeni kwako.
Mwanadada huyu raia wa Zambia ndiye aliyeikamata vizuri chorus ya wimbo huo unaohit sasa hivi.
Lakini nyuma ya sauti hiyo nzuri ya Yvonne, kuna story ya kusikitisha kama ilivyoandikwa kwenye makala ya burudani ya gazeti la Zambia Daily Mail iliyopewa jina la ‘ Yvonne makes waves in Tanzania.’
Dada huyo mwenye miaka 22 ni mtoto wa mbunge wa zamani wa nchini Zambia Michael Mwale na mwanamuziki Jelita Mwanza.
Alianza kujifunza muziki akiwa na miaka saba kwa kuimba shuleni na kanisani.
Muda mfupi hata hivyo, maisha yake yalibadilika baada ya wazazi wake wote kufariki na kumwacha bila chochote kutokana na ndugu kuchukua kila kitu walioacha wazazi wake.
Kwa miaka miwili ilibidi aishi bila makazi rasmi mpaka pale alipopata wasamaria wema waliokuwa tayari kumsaidia.
Pamoja na yote hayo, ndoto yake ya kuwa mwanamuziki wa kimataifa haikupotea na kujikuta akiwa muimbaji mkuu wa Nyali Band iliyoenda kwenye ziara ya Ulaya na sasa yupo Dar es Salaam.
Mwaka 2009 alipata tuzo ya Best Upcoming Artist kwenye Ngoma Awards za nchini Zambia.
Alipokuja mwaka jana kuperform jijini Dar es Salaam Yvonne alilishika sikio la Mzungu Kachaa, aliyemshawishi kuendelea kukaa na kurekodi albam.
Kwa sasa Yvonne yupo chini ya Caravan Records inayomilikiwa na Mzungu Kichaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents