Burudani

Young Killer kuitambulisha ‘MZU’ kwenye wimbo ‘Furaha Yetu’

Rapper Young Killer pamoja na familia yake ya ‘Matunzo Zero Unity’ wanatarajia kuachia wimbo wao wa kwanza.

IMG-20141222-WA0001

Young Killer ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo ni kama zawadi kwa mashabiki na wengine wanaomuunga mkono.

“Wimbo nimefanya Mo Records ni studio ambayo Mwanza inafanya vizuri. Imetoa ngoma nyingi, ngoma karibia zote za Bonta, ngoma za Nako 2 Nako zile. Hii ngoma tumeimba watu wengi kutoka Matunzo Zero Unity. Kwahiyo ni ngoma kwaajili ya mashabiki,” amesema.

“Matunzo Zero Unity ni kama familia ya mashabiki wa muziki wa Young Killer na watu ambao wamesupport muziki wangu. Kwahiyo itaendelea kuwepo milele na milele. Pia video itakuja ila tuanze kwanza na audio.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents