Burudani

Young Killer azungumzia uwezekano wa kuachia album yake ya kwanza

Rapper mdogo kutoka jijini Mwanza, Young Killer Msodoki amedai kuwa yupo kwenye mipango ya kuachia album yake mpya wakati wowote endapo soko litatulia.

Young Killer Msodoki akiwa kwenye hisia
Young Killer Msodoki ( kulia) akiwa na back vocalist wake katika shangwe za Serengeti Fiesta Mwanza

Akizungumza na Bongo5 leo Young Killer amedai kuwa ana nyimbo nyingi ambazo zipo tayari kwa album lakini anasubiria watu ambao wanaangalia masoko ya album.

“Album nina mpango wa kufanya lakini sio sasa hivi kuna vitu ambavyo nasubiria vikae sawa ili nikitoa album niweze kupata mauzo mazuri. Nachelewa kutokana na lawama za watu wanazozitoa kuhusu album halafu nikiangalia asilimia kubwa ya wasanii wengi ni muda mrefu mpaka sasa hivi hawajatoa album. Kwahiyo bado nipo katika udadisi kujua lini nitatoa album yangu,” amesema rapper huyo.

“Kwahiyo nafanya kwanza uchunguzi kuangalia wapi ninaweza kuanzia na kupitisha ila muda wowote ambao nitakuwa na majibu sahihi nitafanya album. Hata mwaka huu kama research yangu ikikamilika mapema muda wowote kuanzia sasa nitatoa album. Sema nimepata taarifa kuna wadau ambao wanakuja sasa hivi wanaboresha soko la album. Kwahiyo mimi nasububiria taarifa yao muda wowote ndipo nitakapofanya surprise ya kutoa album.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents