Burudani

Young Killer ataja faida na hasara za msanii kumweka wazi mpenzi wake ‘Ninaambiwa mimi ni mfano wa kuigwa’

Kuna faida na hasara kwa msanii au mtu maarufu kuweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na Young Killer anatueleza ni zipi hizo.

10362316_695854270498832_253319935_n

“Faida ni kuepuka ule usumbufu ambao kabla hujamtambulisha wanawake tofauti tofauti walikuwa wanakusumbua. Na mpaka sasa hivi wanasumbua lakini nawaambia ‘bwana ingia Instagram angalia picha zangu then wanakuwa wapole,” Young Killer ameiambia Bongo5.

“Hasara ni kuwa kuna wale ambao wanakuwa wameingia moyoni wako deep kabisa wanamtaka Young Killer nadhani kuna baadhi ya mashabiki wanakuwa wanapungua,” ameongeza.

Hata hivyo rapper huyo amedai kuwa kitendo cha yeye kumweka wazi mpenzi wake kimeonekana kama mfano kuigwa.

“Nilishawahi kukaa na msanii mwenzangu akawa anashauriwa kabisa kwamba ‘kwanini na wewe usiwe kama Young Killer, haya mambo ya mademu mademu mpaka lini, kuwa kama Young Killer demu wako mmoja na mambo mengine yanaendelea.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents