Burudani

Young Killer aeleza nia yake ya kuja kuwa Mbunge au Diwani 2025

Rapper kutoka Rock City Mwanza Young Killer Msodoki ameitaja sababu ya yeye kutaja taja Mwanza kwenye ngoma zake kama njia moja wapo ya kutengeneza njia hapo baadaye.

Kupitia kipindi cha Zero Planet ya Ice Fm Msodoki aliulizwa endapo ashapata nafasi ya kuongea au kuitwa na viongozi wa mkoa wa Mwanza kutokana na anavyopeperusha bendera ya jiji hilo kwa mifano ya huko kwa wenzetu Drake alipewa tuzo ya heshima huko Toronto, Fetty Wap pia ashapewa Tuzo hiyo kwa kuitangaza miji yao na Ma-Mea wa miji.

“Siitangazi Mwanza kwasababu ya kuonekana ila nafanya kwa mapenzi yangu mwenyewe familia yangu yote ipo kule na mpaka sasa na wakilisha kule ndiko nimejifunza vitu vingi zaidi pia tutegemee kitu chochote kwenye 2025 huko huwezi jua ishu nzima ya Ubunge au udiwani ndio kitu ambacho….” amefunguka Killer

Young Killer kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake Sinaga Swagga remix aliyofanya na Producer Bin Laden jamaa ambaye anakuja vizuri sana kwa upande wa Hip Hop.

Na Gami Dee (Ice Fm)
Instagram: @gamideetz
Email: [email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents