Michezo

Yaya Toure amtaja mchezaji aliyemshawishi kubaki EPL

Kiungo wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure ameitaja sababu ya kukataa ofa ya mamilioni ya fedha kutoka katika vilabu vya ligi kuu ya China.

Mwanzoni mwa msimu huu Toure (33) alikuwa katika maelewano mabaya na kocha wake Pep Guardiola kitendo ambacho kilimfanya kuondolewa mpaka kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo huku wakala wake Dimitry Seluk akionekana kuchochea zaidi vita hiyo.

Mchezaji huuyo amesema kuwa mshambuliaji wa mahasimu wao Manchester United, Zlatan Ibrahimovic ndiye amemfanya akatae dili hilo ambalo alitakiwa kupokea kiasi cha paundi 500,000 kwa wiki na kuendelea kubaki katika ligi kuu ya Uingereza. “I want to play in Europe, especially in England. I want to continue doing that for a few years yet. Look at my friend Ibrahimovic. He’s 35 and he’s going to play for maybe… three more years?,” amesema Yaya.

“He’s got the same mentality as me. He’s a big player, a champion who loves football. It’s football first,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents