Michezo

Yaya Toure akataa kwenda ligi ya China

Mchezaji wa klabu ya Manchester City Yaya Toure inasemakana kuwa amekataa ombi la mshahara wa paundi 430,000 kwa wiki kutoka China.

Toure ambaye ana umri wa miaka 33 amevutia timu nyingi katika ligi ya China ,wakati ilipoonekana kwamba huenda asishirikishwe katika mechi zozote na kocha Pep Guardiola.

Aliamua kutoondoka wakati huo na akakataa tena alipopewa kitita hicho wakati wa dirisha hili la uhamisho.
Mkataba wa raia huyo wa Ivory Coast unakamilika msimu huu.

Amekuwa mchezaji muhimu wa City tangu aliporudishwa katika kikosi cha kwanza na alianza mechi yake ya saba mfululizo wakati wa kushindwa kwa 0-4 dhidi ya Everton katika mechi ya ligi ya Uingereza hapo Januari 15.

Toure amekuwa huru kuingia katika mkataba na vilabu vingi ughaibuni tangu mwezi Januari lakini imedaiwa kwamba bado anapenda ligi ya Uingereza.

Toure bado hajapata hakikisho lolote kuhusu mkataba wake kutoka kwa kocha wake Guardiola.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents