Burudani

Yaya awashtaki Mariah Carey na Nick Cannon, asema alifukuzwa kwakuwa watoto wao walimpenda kuzidi mama yao

Mariah Carey na Nick Cannon wanaweza kuwa wanapeana talaka lakini bado wana jambo la kujibu pamoja kwakuwa wameshtakiwa na yaya wao wa zamani kwasababu tu alionesha upendo mwingi kwa watoto wao mapacha.

GTY_nick_canon_mariah_carey_kids_sk_140109_16x9_992

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Simonette DaCosta anadai kuwa alikuwa yaya ‘full-time’ wakati watoto hao walipokuwa watoto ambapo aliwalisha, aliwaogesha na kuwabembeleza lakini hilo halikumpendezesha Mariah.

DaCosta anadai kuwa muimbaji huyo alimkosoa kwa kuwapenda mno wanae hiyo ikimaanisha kuwa Mariah aliingiwa na wivu sababu watoto wake walimpenda yaya kuliko yeye.

DaCosta pia anadai kuwa alikuwa akifanya kazi nyingi mno na kudai kuwa alikuwa akitumia saa 100 kwa wiki kufanya kazi.

Anataka alipwe gharama mbalimbali ikiwemo hasara aliyopata.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents