Habari

Yampasa Rais kuwasikiliza watu waliompigia kura – LHRC

Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kimesema kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuzivamia ofisi za Clouds Media Group akiwa na askari wenye silaha.

Akizungumza na wanahabari Jumanne hii mkurugenzi wake mkuu, Dk Helen Kijo-Bisimba ametoa wito kuwa serikali imchukulie hatua za kinidhamu na kijinai mkuu huyo wa mkoa.

“Hili suala la uwajibikaji kwasababu ni mamlaka ya Rais anasema yeye ndio anayechagua na yeye anaweza kufuta. Lakini Rais huyu ni wa kwetu sisi pamoja na kwamba alichukua form mwenyewe lakini alipigiwa kura lakini na hata wale ambao hawakumpigia kura walikubali hawakugoma. Si unajua kuna wakati mtu unaweza ukapigiwa kura na watu wakakataa na nishawahi kuona nchi moja Mauritius mtu alichaguliwa akaondolewa na watu walioandamana, sasa huyu ambaye alichaguliwa na watu wakakubali hawakugoma na akapewa,” amesema.

“Rais kwahiyo itabidi awasikilize watu waliompa kura itabidi awasikilize, kuwasikiliza ni watu kuongea lakini tukiendelea na hii tabia ya uoga hatusemi mambo hayataendelea. Na mimi nadhani raia wa Tanzania wana uwezo wa kumshinikiza Rais au huyo aliyekosea ambaye ni mkuu wa mkoa aondoke na moja wapo tunaweza kuacha kufanya naye kazi, anaenda kutufungulia madaraja ya nini kama anaweza kutuletea matatizo ya kihuni tunaacha kufanya naye kazi.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents