Burudani

Wolper atoa sababu iliyomfanya apunguze kuvaa nguo za kiume

Kweli ujana ni maji ya moto. Mwigizaji kutoka kiwanda cha filamu bongo, Jacqueline Wolper amesema mchumba wake ndiye sababu iliyomfanya apunguze kuvaa nguo za kiume.

Wolper akiwa hana pete ya uchumba

Miaka kadhaa nyuma CV ya Wolper ilichafuliwa na skendo zilizokuwa zinamiuandama kuwa yeye ni msagaji japo mara nyingi mwenyewe amekuwa akizikana hizo taarifa kuwa hazina ukweli wowote.

Akiongea kwenye kipindi cha Nirvana, kinachoruka kupitia EATV, Wolper alisema ‘nilikuwa navaa vile kutokana na wakati ule, sasa hivi nimeshakuwa na mchumba’.

“Nilikuwa navaa vile kutokana na wakati ule ulivyokuwa. Kuna watu walikuwa wanapenda, lakini sasa hivi nimeshakuwa mchumba wa mtu. Ni kweli lazima nivae gauni, kwahiyo mtu unatakiwa ujibadilishe wewe mwenyewe usisubiri kubadilishwa,” aliongezea.

Wolper aliendelea kusema, “hata hivyo bado sijaacha kabisa, kidogo unakuwa unagusia mashabiki zako wanakuwa wanakupenda.”

Hata hivyo Wolper japo amekiri kuwa na mchumba mpya kwa sasa lakini hayupo tayari kuweka mahusiano yake hadharani kama mwanzo alivyokuwa anafanya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents