BurudaniDiamond Platnumz

Wolper adai kuna filamu inakuja akiwa na Diamond

Jacqueline Wolper anaweza kuwa kimya kwenye filamu kwa kipindi kirefu lakini ana mipango mikubwa kwenye tasnia hiyo.

13167199_1038803779540713_504515015_n

Muigizaji huyo amedai kuwa na mpango wa kuja na filamu aliyoshirikiana na ex wake Diamond Platnumz. Wolper ambaye kwa sasa ni mpenzi wake na Harmonize, alikiambia kipindi cha Take One cha Clouds TV wiki hii kuwa pamoja na kwamba aliwahi kuwa na uhusiano na staa huyo na kisha kuachana, bado wamebaki kuwa washkaji wa nguvu.

Alisema ukaribu wao ni zaidi ya urafiki na wameendelea kushirikiana katika mengi. Ni kweli kwakuwa Wolper ndiye ex wa Diamond pekee aliyeonekana kwenye video ya Utanipenda.

Hata hivyo hakusema ni lini filamu hiyo itaanza kufanyiwa maandalizi. Kama itakuwepo, hiyo itakuwa filamu ya kwanza ya Diamond.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents