Burudani

Wizkid na Victoria Kimani washoot video Kenya na Enos Olik

Staa wa Nigeria Wizkid amekuwepo Afrika Mashariki kwa takribani wiki moja. Alianzia jijini Nairobi Kenya ambapo Jumapili iliyopita alitumbuiza kwenye viwanja vya The Carnivore, na baadae kuelekea jijini Kampala Uganda ambako alitumbuiza kwenye Party ya Guiness na kisha akarudi tena Kenya ambako imefahamika alirudi kushoot video.

Wizz
Victoria Kimani (kushoto) Wizkid (Kulia)

Staa huyo wa ‘If I Show You My Money’ ameshoot video nchini Kenya na director Mkenya Enos Olik ambaye amewahi kufanya video za wasanii wa Bongo kama Weusi (Gere), Vanessa Mdee (Come Over) na video mpya ya Shaa (Njoo).

Wizkid ameshare picha Instagram akiwa na Victoria Kimani na kuandika:

Wiz and Vicy2
“Videoshoot in Kenya!! Big up @iamdelb @victoriakimani nd @patrickelis !! Thank u Nairobi u have been good to us. We off!”

Director Enos Olik amethibitisha juu ya uchukuaji wa video ya Wizkid kwa kushare picha akiwa nae na kuandika:

Wiz and Olik
“Me and my bro @wizkidayo About to kill it on Set…#MusicVideoTings
#Kenya #Naija #Connection . #BokehFamily “

Victoria Kimani ambaye pia anaonekana kuhusika kwenye video hiyo nae ameshare picha na kuandika:

Wiz and Vicy
“Video shoot fresh @wizkidayo”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents