Habari

Wizkid na Diamond wameipoteza tuzo ya BET kwa Black Coffee, nguli wa SA asiyestahili kupuuzwa

Mshindi wa BET Awards 2016, kipengele cha Best International Act: Africa ni Black Coffee wa Afrika Kusini.

image

Ushindi wake umeshangaza wengi. Waliokuwa wanatarajiwa zaidi kushinda tuzo hiyo ni Diamond na Wizkid. Na kwa mashabiki wengi wa Diamond, Wizkid ndiye waliyekuwa wakimhofia zaidi. Lakini tulikuja kujipa moyo kuwa huenda mwaka huu ushindi ni wetu kutokana na msimamo wa Wizkid dhidi ya tuzo hizo za Wamarekani.

Mwaka jana alieleza sababu ya kutohudhuria akidai kuwa haziwapi heshima wasanii wa Afrika na UK. Na tangu atajwe kuwania tuzo hizo, hajawahi kujali,  kusema chochote na hakuhudhuria kabisa. Hivyo nafasi kubwa ilionekana kwenda kwa Chibu. Hata hivyo, BET waliamua kumpa Black Coffee – Dj ambaye jina lake ni geni kabisa kwa Watanzania wengi.

image

“For the past 4/5 years I have been doing tours outside my Country…..in the last two years even relocating my Family with me while on tour to make everything work…..Taking our South African Music to places I can’t even pronounce,” aliandika kwenye Instagram baada ya ushindi huo.

“I’m Greatful to my lady @enhlembali_  and my kids for allowing me to chase my dreams unconditionally…….my great team @amarudacosta @lionelmarciano and both offices in SA and NY….Universal Music team in SA…..Ultra Music team in NY and the William Morris Team in LA…..a BET  Award comes to our our Land for the first time.This is a Great Honour…..We did not do this alone…Thank you for all your Votes…..Thank you for the Love. #betawards16 #bestinternationalaact2016 #gotnothingbutloveformypeople #southafica #onemanband #Godsveryown #california #itsallpossible,” aliongeza.

Diamond alimpongeza pia kwa ushindi huo. Lakini pamoja na jina lake kutokuwa kubwa katika upande mwingine wa Afrika, ukitoa Kusini, Black Coffee ni legend ambaye katika wote aliokuwa ametajwa nao, yeye ndiye kaka yao.

Black Coffee ni nani?

image

Jina lake halisi ni Nathi Maphumulo. Ni Dj mwenye mkono mmoja. Alipoteza mkono wake baada ya taxi kuanguka kwenye kundi la watu ambalo naye alikuwemo, mtu mmoja alikufa na Black Coffee alikuwa mmoja wa watu 36 waliojeruhiwa.

Ajali hiyo ilimfanya Maphumulo apoteze mkono mmoja ambao umejikunja kama ngumi na kuwa mfukoni mara nyingi. Mkono wake wa kushoto siku zote huwa upo mfukoni na bado akiwa na miaka 35, amefanikiwa kuwa na mafanikio ambayo wengi katika umri huo hawana.

Lakini hakukata tamaa ya kuwa DJ mkubwa ambapo alijiunga na chuo cha Durban Tech kusomea music production.  Kwa sasa Black Coffee ni mmoja wa majina yanayoheshimika kwenye muziki wa dance nchini Afrika Kusini na kimataifa pia.

Black Coffee hajawahi kutaka kujulikana kama ‘DJ mwenye mkono mmoja’ kwakuwa anapenda atambulike kwa kipaji chake na sio kwa ulemavu wake. Alifungua label yake iitwayo Soulistic Music na ameshacheza muziki katika maeneo mengi yakiwemo Uingereza, Marekani, Ugiriki na kwingine duniani na huko anaheshimika mno.

Black Coffee kwa sasa anaichukulia hali yake kama baraka iliyokuja na wajibu kwakuwa kila anachokifanya huwakilisha walemavu. Ana taasisi yake ya The Black Coffee Foundation ambayo huchangia senti 5 ya kila CD anayouza.

Mwaka 2010, alipiga muziki kwa saa 60 mfululizo kwaajili ya kuingia kwenye The Guinness Book of Records kama DJ mwenye mkono mmoja aliyepiga muziki kwa muda mrefu zaidi ili kuchangia taasisi hiyo.

Miezi miwili iliyopita, Black Coffee alienda Marekani ambapo miongoni mwa mambo aliyoyafanya ni kualikwa kwenye house party ya Diddy na kutumbuiza, tena ladha za Afrika.

Diddy alishare kwenye Instagram video ya DJ huyo na kuandika: The best music at #ultra is HERE!! The World Famous @realblackcoffee bringing the Africa vibrations live from #BlueDotUltraWeekend!!#LetsDance #PositiveVibesOnly.”

Naye Black Coffee alirepost video hiyo na kuandika: What a Party!!!!!!what a Legend!!!! Thank you for hosting us @iamdiddy @cassie. Year of the Underdog by @culoedesong #Bless.”

Kama hiyo haitoshi, Coffee alisaini mkataba na label maarufu ya Marekani, Ultra Records nyumbani kwa wasanii wakubwa wa muziki wa house wakiwemo  David Guetta, Pitbull, Calvin Harris, na  Benassi.

11098343_986371191436966_1158589434_n
Black Coffee akiwa na uongozi wa Ultra Records

Coffee ametoa album yake mpya New Pieces Of Me kupitia label hiyo.

Lakini muhimu ni kwamba tuzo hizi zisitugawe Waafrika. Na hakika maneno ya Cassper Nyovest aliyekuwa akiwania pia kipengele hicho ni ya muhimu zaidi.

“African pride!!! Shout out to all the nominees and the winners!!! Let’s grow with love and God. You’re all beautiful and I love you from the bottom of my heart!!! My brothers and sisters!!! #Family #AfricaNa1.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents