Habari

Wizkid adaiwa kukamatwa Nairobi, ni baada ya kupatikana akivuta bangi hotelini

Staa wa Nigeria, Wizkid ambaye alikuwa nchini Kenya kushoot video na Victoria Kimani, anadaiwa kukamatwa na polisi katika hoteli ya Nairobi Crown Plaza, Jumamosi mchana na kuhojiwa kwa masaa kadhaa kabla ya kurejea Lagos, Nigeria.
Wizkid-pic

Kwa mujibu wa Pulse Magazine la Kenya, Wizkid alikamatwa akivuta bangi ndani ya hoteli hiyo kitu ambacho hakiruhusiwi. Ofisa mmoja wa hoteli hiyo alimuuliza kwanini anavuta bangi ndani ya hoteli hiyo na hivyo wakajikuta wakiwakiana na walinzi kuingilia kati kabla ya polisi kuitwa na kumkamata.

kabla ya kupelewa kwenye kituo cha polisi cha Capital Hill ambako alihojiwa, hoteli hiyo ilimpiga faini ya shilingi 50,000 za Kenya ambazo alizilipa kwa credit card.

Victoria Kimani ndiye aliyemsaidia kumtoa kituoni hapo. Wizkid alitakiwa kuondoka saa tisa mchana siku hiyo lakini kutokana na drama hiyo aliahirisha safari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents