Burudani

Witness: Kila mtu anatakiwa kubrand maliasili zetu zisipotee

Kuanzia wiki iliyopita kwenye mtandao wa Twitter kumeonekana kuwa hapatoshi kwa kuwa busy sana baada ya Witness a.k.a Kibonge Mwepesi kuanzisha kampeni ya kwenye mitandao kwa kuzitangaza maliasili zetu zilizopo Tanzania zisipotee.

1966176_10203127404337184_581002193_o

Akiongea na XXL ya Clouds FM, Witness amesema, “Kubrand maliasili zetu ni jukumu la kila mtanzania siyo kwa serikali tu peke yake, nchi nyingine wananchi wake wanajitahidi kutangaza maliasili zao mpaka wanapitiliza mipaka kwa kuiongopea dunia kwa kusema baadhi ya vitu vyetu vipo nchini kwao.”

Sakata hili la kutangaza maliasili za Tanzania limekuja juu baada ya kuonekana kipande cha video ikimuonyesha mdada aliyejulikana kama Rosemary Odinga ambaye ni mtoto wa aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Kenya akisema kuwa Olduvai Gorge ipo nchini Kenya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents