Burudani

Wimbo wa Alikiba ‘Mwana’ wafikisha views zaidi ya laki 1 Youtube ndani ya wiki 3

Mapokezi ya Alikiba kupitia wimbo wake mpya ‘Mwana’ aliouachia wiki tatu zilizopita ni ishara njema kwa msanii huyo, kuwa bado ana mashabiki wengi ambao wanaweza kumvusha na kumfikisha anakotarajia kufika.

http://youtu.be/cllJK5AMJf0

Audio ya wimbo huo ambayo pia iliwekwa kwenye mtandao wa video wa youtube, ndani ya wiki tatu toka iwekwe imeweza kupata views zaidi ya laki moja (105,375).

Kupitia Instagram Alikiba amewashukuru mashabiki kwa mwanzo huo wa mafanikio.

kiba

“Ahsante Fredrick na wengine wote mliopokea #Mwana (audio) hivi.
July 25, 2014 hadi leo na ndani ya wiki 3 hits zaidi ya 100,000!
Ahsanteni sana kwa support yenu!”
Aliandika Alikiba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents