Burudani

Wimbo mpya wa Shaa ‘Toba’ umeandikwa na muimbaji wa ‘Mchumba’ H.Mbizo

Aliyeandika wimbo mpya wa Shaa ‘Toba’ uliotoka wiki hii, ni msanii wa muda mrefu aitwaye H.Mbizo.

Shaa uhindi

H.Mbizo ni msanii aliyewahi kufanya vizuri miaka ya nyuma na wimbo wake uitwao ‘Mchumba’.

Said Fella ameiambia Bongo5 kuwa Mbizo aliuandika wimbo wote miaka miwili iliyopita na kutayarishwa na producer wa Nigeria aitwaye Big H.

Ameongeza kuwa wengine waliohusika na utayarishaji wa wimbo huo ni producer Shirko pamoja na shemeji Master Jay.

Katika hatua nyingine Shaa kupitia gazeti la Mtanzania ameelezea jinsi alivyopata wazo la video ya wimbo huo iliyofanywa na director Justin Campos wa Afrika Kusini.

“Video nilipata wazo la kuifanya iwe katika mwonekano wa Kihindi nilipopeleka wazo langu kwa ‘director’ wa video yangu akamtumia mke wake wananikutanisha na kundi la wanenguaji wa asili ya Kihindi tukafanya video nzuri ambayo kwa sasa imeanza kufanya vizuri kupitia vituo mbalimbali vya redio na televisheni,” alifafanua Shaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents