Habari

WHO: Nigeria haina tena Ebola

Shirika la afya duniani, WHO, leo limetangaza kuwa Nigeria haina tena ugonjwa wa Ebola.

ebola-virus-close

Hatua hiyo imedaiwa kama ushindi na shirika hilo.

Nigeria iliripoti kesi 20 za Ebola pamoja na vifo nane tangu ugonjwa huo ulipuke. Miongoni mwa watu waliofariki ni pamoja na abiria wa ndege aliyeupeleka ugonjwa huo nchini Nigeria na kufariki baadaye kidogo.

Ugonjwa huo bado unaendelea kusambaa kwa kasi katika nchi za Liberia, Sierra Leone na Guinea na umeshaua zaidi ya watu 4,500.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents