Burudani

Weusi wapanga kujenga maktaba 100 nchini kote ili wanafunzi wajisomee

Weusi wanaendelea kufikia ‘Nje ya Box’ kila kukicha. Kundi hilo linatarajia kushirikiana na Watanzania kujenga maktaba 100 katika vijiji mbalimbali vya Tanzania ili kuwahamasisha wanafunzi kujisomea.

Weusi wakifanya yao

Msemaji wa kundi hilo, Nick wa Pili ameiambia 255 ya kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa kundi hilo lilikuwa na mpango huo kwa miaka mingi na sasa unakaribia kutimia.

“Tumekaa tukafikiria tufanye kitu to give back to the community,” alisema. “Toka zamani mimi nilisemaga na idea yangu ya kijiji cha taaluma ambacho ni kutambua machimbo ambayo yako uswahilini ambayo wanafunzi wanasoma na kuyafacilitate. Lakini sasa hivi nikaona hii idea ime expand lakini nikatafuta msemo ambao uko uswahilini vijana wa kawaida ambao ni watu wa chini kabisa kwa sababu sisi watu wa chini kwa mfumo wa maisha yetu kuna matatizo ambayo sisi tunachangia sisi kuyatekeleza. Kwahiyo hiyo kampeni inaitwa ‘Mia Mia Mwanangu’ ni kampeni rahisi sana inajaribu kuhamasisha kila mtu au mtu mwenye uwezo wa kuchangia shilingi mia, lengo tunataka tutengeneze maktaba ndogo mia katika vijiji mia, na kila maktaba itakuwa na vitabu mia. Kama kamaktaba kadogo tu ambako katakuwa na vitabu mia, ambapo sasa hivi tunafanya maongezi na solar tukifanikiwa jamaa solar kwa sababu na wao wanatangaza bidhaa zao wanaweka solar pale,” aliongea.

“Nimeweka shilingi mia kwa sababu hii itagusa watu wa chini, kutaka watu wa chini wa-take action wenyewe kwa ku-support elimu na kuleta changes kwa sababu tumezoea kuona NGO mpaka msaada utoke Ulaya au watoe msaada wakubwa wenye uwezo. Ila sisi watu wa kipato cha chini tunaweza kusababisha kuleta mabadiliko kwenye jamii, kampeni sasa hivi tunafukuzia regulation halafu pia tuna maongezi na jamaa wa solar.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents