Michezo

Wenger: Siwezi kusoma kitabu cha Mourinho

Kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ”hatosoma” kitabu ambacho kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema atauvunja uso wa kocha huyo wa Arsenal.

_91356707_wenger_mourinho_rex

Mourinho amekuwa akizozana na Wenger mara kwa mara alipokuwa akiifunza Chelsea na alimuita mkufunzi huyo ”maalum kwa kushindwa”.

”Mimi huzungumza kuhusu soka-hicho ndio ninachofanya”,alisema Wenger mwenye umri wa miaka 66.

”Siko katika hali ya kutaka kuharibu,mimi hupenda kujenga.Ninaangazia mechi ya Jumamosi dhidi ya Chelsea”.

Mourinho mwenye umri wa miaka 53 alimuita Wenger ”mpiga chabo” mwaka 2005 baada ya kutaka kujua kuhusu sera za uhamisho za Chelsea.

Mourinho alimuita Arsene Wenger ”mtu maalum kwa kushindwa”,mnamo mwezi Februari 2014 baada ya raia huyo wa Ufaransa kusema kuwa baadhi ya wakufunzi wa ligi kuu ya Uingereza wameanza kulalamika kwa sababu ”wanahofia kufeli”.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents