Michezo

Wenger amkana Henry mbele ya waandishi

Kocha wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger amewaambia waandishi kuwa mchezaji wa zamani wa timu hiyo Thiery Henry hajawahi kukutana na hasira za mashabiki 60,000.

thierryhenryarsenewenger-cropped_1viel1jtdbz1n1degssu7ceb17

Baada ya timu ya Arsenal kufungwa wakiwa uwanja wao wa nyumbani kwa magoli mawili kwa moja dhidi ya Swansea, mchezaji nguli wa Arsenal, Thiery Henry alisema, “Sijawahi kuona mashabiki wa Arsenal wana hasira kiasi kile baada ya kufungwa na Swansea kwenye uwanja wao nyumbani.”

Kwenye mkutano na waandishi wa habari kocha Arsene Wenger alisema, “Henry hajakutana na hasira za mashabiki 60,000 moja kwa moja kwasababu yeye kwanza anakaa kwenye viti bora vya gharama ambapo hakuna mashabiki wenye hasira huko anapokaa. Hayo ni mawazo yake lakini hajakutana mara nyingi na kiwango cha hasira cha mashabiki.”

Kocha huyo pia aliongeza kwa kusema, “Hayo ni mawazo yake na ni haki yake, mashabiki wataendelea kuwa nyuma yetu na sina wasiwasi juu ya hilo. Siku zote kwenye soka tunafanya 98% na tunahitaji kutafuta hizo 2%.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents