BurudaniDiamond PlatnumzWema Sepetu

Wema Sepetu avunja rekodi ya Instagram Kibongobongo

Picha ya Diamond Platnumz inayomuonesha akiwa amelala na huku shavuni kukiwa na lipstick za mwanamke iliyowekwa kwenye ukurasa wa Instagram wa Wema Sepetu, imevunja rekodi ya mtandao huo kwa Tanzania kwakuwa na comments nyingi zaidi.

30be5d5eabd811e38f071285a6421f42_8

Hadi sasa picha hiyo ina comments 1,786 na hivyo kuizidi picha nyingine aliyoiweka mwezi uliopita ambayo ndio ilikuwa picha ya kwanza inayomuonesha Wema akiwa na Diamond tangu warudiane. Picha hiyo ilipata comments 1,601.

Wakati huo huo Diamond ndiye staa wa Afrika Mashariki mwenye followers wengi zaidi kwenye Instagram (ukimtoa Lupita Nyong’o mwenye followers 930,744, au wengine wanaoishi diaspora). Hadi sasa staa huyo ana followers 95,900+ akifuatiwa na mpenzi wake Wema mwenye followers 82,870+.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents