BurudaniDiamond PlatnumzWema Sepetu

Wema hajampeleka Diamond mahakamani – Martin Kadinda

Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini likiwemo gazeti la Mtanzania kuwa amempeleka Diamond polisi kwa kile kinachosemwa ni kumtapeli shilingi milioni 10.

wema na diamond

Martin ameiambia Bongo5 kuwa Wema na Diamond hawadaiani chochote na kwamba habari hizo ni za uongo.

“Unajua tatizo ni kwamba hatujajua source ni nani,” amesema Martin. “Kwa sababu taarifa ikishaingia kwenye social network everybody posts, kwahiyo sisi tunamtafuta nani ameianzisha hiyo stori. “We don’t have any issue with Diamond. Diamond hana issue yoyote na Wema,” amesisitiza.

“Kwahiyo tunashangaa ni kama ambavyo wanazusha sijui kafumwa na nani ni uongo mtupu. Lakini nashangaa media ambazo zinaaminika zinaamua kuandika story bila kumpigia simu mhusika au meneja na kuuliza ukweli wa hiyo story.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents