Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Burudani

WCB ya Diamond kumsaini Q Chief?

By  | 

Label kubwa ya muziki nchini, WCB ya Diamond Platnumz, huwenda ikamsaini msanii mkongwe wa muziki nchini Q Chief.

Muimbaji huyo aliyewahi kufanya vizuri na wimbo ‘Si Ulinikataa’ hivi karibuni alitembelea katika ofisi za WCB na kufanya mazungumzo na uongozi wa label hiyo.

Akiongea katika kipindi cha Yaliyomoyamo cha Radio One Stereo Jumatano hii, Q Chief amedai hivi karibuni alikuwa kwenye mazungumzo la label kubwa ya muziki nchini Tanzania.

“Tayari nimenza kuyaa approach makampuni makubwa sana,” alisema Q Chief. “Kuna uwezokano nikasaini na mmoja ya wadogo zangu ambaye anafanya vizuri kuliko msanii yeyote hapa nchini,”

Aliongeza, “Lakini si nasaini kwa sababu mimi ni mjinga, nasaini kwa sababu nataka kuudhihirisha mimi ni Abubakar Katwila na hakunaga Abubakar Katwila mwingine,”

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri wa wimbo Sungura.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW