Habari

Waziri Mkuu wa Italia apanga kujiuzulu kwenye nafasi hiyo

Waziri Mkuu wa Italia Matteo Renzi ametangaza kuchukua maamuzi ya kujiuzulu baada ya kushindwa kwenye kura ya marekebisho ya katiba ya nchi hiyo.

42yw4xode6dln7zpdtx9wlfonxfmreay-large

Akiongea na waandishi wa habari kiongozi huyo alisema anakubali lawama kutokana na matokeo hayo na amekubali kuwa kambi ya upinzani iliyokuwa ikipinga mageuzi hayo kutoa pendekezo la mwelekeo kuanzia sasa.

“Good luck to us all,” Renzi aliwaambia waandishi wa habari baada ya kumaliza mkutano huo.

Waziri huyo alifanikiwa kupata kura asilimia 40 zilizokuwa zikimuunga mkono kwenye mapendekezo yake hayo huku upande wa upinzani waliokuwa wakimpinga walifanikiwa kushinda kwa asilimia 60.

Hata hivyo Waziri huyo ameongeza kuwa atamuandikia barua yake ya kujiuzulu Rais wa nchi hiyo Sergio Mattarella baada ya kikao chake cha Jumatatu hii na mawaziri wa upande wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents