Habari

Waziri Mkuu: Serikali italinda amani kwa gharama yoyote

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itahakikisha inalinda amani ya nchi kwa gharama zozote na kamwe haitoruhusu mwanasiasa yeyote kusababisha vurugu zitakazochochea uvunjifu wa amani.

DSC_1818

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kuwaondoa hofu wananchi kuwa serikali haitakubali mwanasiasa yeyote kuharibu amani.

“Ni kweli kuna viashiria, lakini nataka kukuhakikishia kwamba serikali tumesimama vizuri hatutaruhusu mwanasiasa yeyote atakaye sababisha vurugu nchi hii, kimbilio la katiba sijui tunaruhusiwa hapana hakuna jambo ambalo halina mipaka”,alisema Majaliwa.

Mheshimiwa Majaliwa alielezea kauli mbiu ya Rais amesema “kauli ya Rais Magufuli ya ‘hapa kazi tu’ ilikuwa sio neno la mchezo na kwamba lina maana kuwa watu wafanye kazi zinazowaletea tija.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents