Habari

Waziri Mkuu: Serikali haijakumbwa na baa la njaa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema nchi haijakumbwa na baa la njaa na amewataka Watanzania kutosikiliza kampeni za upotoshwaji zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiashara kuhusu hali ya chakula kwani si za kweli bali ni za uzushi zenye lengo la kupandisha bei za vyakula.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo Jumatatu hii wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa mara baada ya kuzindua safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.

“Naomba wananchi msiwe na wasiwasi juu ya hali ya chakula nchini, msisikilize kelele zinazopigwa na watu mbalimbali pamoja na kwenye baadhi ya vyombo vya habari yakiwemo magazeti kwani taarifa hizo si za kweli. Chakula kipo cha kutosha licha ya mvua kusuasua katika baadhi ya maeneo nchini,” amesema Majaliwa.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents