Siasa

Waziri Mkuu azungumzia Matukio ya watu Kutekwa na Kupotea

By  | 

Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema Serikali imesikia matukio yote yanaondelea nchini na kuwataka Watanzania kuwa watulivu na kuipa serikali na vyombo vya ulinzi muda.


Pichani: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo katika Mkutano wa Saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linaloendelea mjini Dodoma, kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo ya wabunge kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani, Mbunge wa Hai, Mh. Freeman Mbowe (Chadema), alipata nafasi ya kumuuliza waziri Mkuu swali kuhusu hali ya usalama nchini.

Watanzania wamekuwa na hofu juu ya watu kupotea, watu kutekwa huku mambo mengi yakiendelea kwenye mitandao, na mijadala katika vyombo vya habari. Msaidizi wangu, Ben Saanane alipotea ghafla,na Serikali haijawahi kutoa kauli yoyote kuhusu hilo, na sielewi nini kinafanyika, Jambo ambalo linaloonyesha aidha serikali haitaki kufanya uchunguzi wa kina, au imeshindwa kufanya uchunguzi, Je? Mh. waziri mkuu unaipa kauli gani Taifa kuhusu suala hili?.
Na Emmy Mwaipopo

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments