BurudaniMichezo

Waziri Mkuu awapongeza mwanariadha Felix Simbu, Diamond na Serengeti Boys kwa kuipa sifa Tanzania

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, jana aliwapongeza mwanariadha Alphonce Felix Limbu, staa wa muziki, Diamond Platnumz na Serengeti Boys kwa kuiletea sifa Tanzania hivi karibuni.

Mheshimiwa Majaliwa alitoa pongezi hizo bungeni mjini Dodoma wakati akiahirisha mkutano wa bunge hilo. Alisema serikali itaendelea kuhamasisha uwezekaji kwenye shughuli za michezo na burudani kama moja ya maeneo ya kutengeneza ajira kwa vijana.

“Kwanza mwezi January mwaka huu 2017, Mtanzania mwenzetu Alphonce Felix Simbu aliibuka mshindi wa kunyakua medali ya dhahabu kwenye mashindano ya riadha ya dunia ya Mumbai Marathon,” alisema Waziri Mkuu.

“Lakini mbili, Mtanzania mwezi Naseeb Abdul, maarufu kama Diamond Platnumz alipata heshima ya kutumbuiza kwenye ufunguzi wa fainali za kombe la Afrika lililomalizika hivi karibuni nchini Gabon,” aliongeza.

Pia aliwapongeza vijana wa timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys kwa kufuzu kwenye fainali ya kombe la Africa nchini Gabon.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents