Habari

Waziri Mbarawa aahidi kubadili uongozi wa juu wa shirika la Posta

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ameahidi kubadilisha uongozi wa juu wa shirika la Posta nchini kutokana na kushindwa kuendeleza shirika hilo kwa kasi inayotakiwa.

Waziri huyo ameyasema hayo jana alipofanya ziara katika ofisi za shirika hilo za Posta jijini Dar es Salaam na kujionea shughuli zikifanyika na baadaye kuzungumza na wafanyakazi Makao Makuu ya TPC.

“Unajua ifikie mahali tuambizane ukweli, tukianza kuogopana hapa kwamba kesho nakuletea hela, hakuna hela, hela mnayo mna maghorofa kwanini hamfanyi kazi, tumeenda asubuhi posta hapa , posta nzima ina wateja 20 ni aibu. Mnakaa mnafanya nini hamuendi kutangaza Posta, hamuhangaiki kutafuta wateja,” alisema Nbarawa.

“Ni lazima kufanya uamuzi. Inawezekana mzazi wako amefariki na amekuachia mali nyingi hivyo usipozitumia unakuwa masikini, shida yenu Posta ni uongozi. Hamjapata viongozi wa kusimamia Posta, sisemi hivyo kwa kuwa namwonea mtu bali ni hali halisi,” alisema Mbarawa.

Aidha Waziri Mbarawa alisema, atamtafuta mtendaji mzuri na kumpeleka ili shirika liwe na mabadiliko kama alivyofanya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Shirika la Meli kwa kupeleka watendaji wenye maono ya mbali.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents