Michezo

Wayne Rooney: Man United itafuzu ligi ya mabingwa Ulaya

Mchezaji wa klabu ya Manchester United na nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney amedai kuwa timu yake ipo kwenye nafasi nzuri kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya Uefa ifikapo mwisho wa msimu.

Manchester United wanashika nafasi ya sita kwa sasa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Uingereza, lakini wamepunguza pengo la alama dhidi ya timu zinazoshika nafasi za nne za mwanzo baada ya kucheza mechi 15 bila kufungwa.

United bado wamo kwenye Ligi ya Europa, Kombe la FA na lile la EFL, na Rooney anaamini kwamba wapo kwenye nafasi nzuri kufurahia mafanikio ya msimu.

“Nadhani mambo yanakwenda sawa. Tupo kwenye nafasi nzuri kutinga nne bora. Ni dhahiri malengo yetu yalikuwa kujaribu kuwa mabingwa, jambo ambalo ni gumu kwa sasa. Tunalitambua hilo. Lakini bado tupo sehemu nzuri katika harakati zetu za kutinga nne bora,” Rooney aliliambia gazeti la GQ.

“Bado tumo kwenye Europa, Kwenye fainali ya Kombe la Ligi, na kwenye Kombe la FA, kwa hiyo tunaamini ni mataji ambayo tuna uwezo wa kutosha kuyatwaa. Kisha tutamaliza ndani ya nne bora kwa upande wa ligi.

“Jose Mourinho ni wazi kwamba ni meneja bora – nadhani rekodi zake katika klabu zote alizofundisha zinadhihirisha hilo. Nadhani anajua kile anachokitaka kutoka kwa wachezaji, na wachezaji wanafahamu meneja anachotaka kutoka kwao. Ni mtu thabiti na mwema iwapo utatimiza majukumu anayokupatia.

United watakuwa nyumbani katika uwanja wao wa Old Trafford Jumamosi hii wataikaribisha Watford katika wakijua kwamba ushindi unaweza kuwapandisha hadi nne bora kutegemeana na matokeo ya timu nyingine.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents