Michezo

Wayne Rooney kusaini mkataba mpya na Man United wiki hii, atakuwa akilipwa tshs mil 793 kwa wiki

Wayne Rooney atasaini mkataba mpya na klabu yake ya Manchester United wiki hii ambapo atakuwa akilipwa £300,000 kwa wiki ambazo ni sawa na shilingi milioni 793,800,000.

Rooney (640x640)

Mkataba huo utamfanya Rooney kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi kwenye historia ya soka la England. Kwa sasa Rooney yupo Dubai pamoja na kikosi cha David Moyes walikoenda kujifua na mkataba huo atausaini rasmi wakirejea England baadaye wiki hii.

Kubaki kwa Rooney kwenye klabu hiyo kunaonekana kama ushindi kwa Moyes kwakuwa mchezaji huyo alikuwa ana nia ya kujiunga na Chelsea waliokuwa wametoa ofa mbili zilizokataliwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents