Habari

Watu wasiopata kifungua kinywa (breakfast) wana hatari ya kupata magonjwa ya moyo

Wote tunafahamu kwa muda mrefu kile unachokula ndicho kinachofanya uwe hivyo jinsi ulivyo kuanzia ndani mpaka nje. Ukila vyakula vyenye mafuta mengi (fatty foods) mwisho wa siku utakuwa mnene.

Lakini sidhani kama unafahamu muda unaokula chakula chako pia una matokeo ya moja kwa moja kwenye afya yako? Ripoti nyingi zimetanabahisha kwamba 27% ya wanaume ambao hawanywi kifungua kinywa (skipping breakfast) wana hatari kubwa ya kupata shambulio la moyo (heart attack) au kifo kutokana na magonjwa ya moyo kuliko wale ambao wamekuwa wakipa kifungua kinywa kila siku.

Pia imeripotiwa kuwa wanaume ambao huchelewa kula chakula cha jioni/usiku (eating late at night /eating after going to bed) wana asilimia 55 (55%) ya zaidi ya kupata magonjwa ya moyo (coronary heart disease) kuliko ambao wanakula katika mUda muafaka.

“Kutopata kifungua kinywa (Skipping breakfast) inakusababishia kuwa katika hatari ya kupata shikizo la damu, kisukari, unene uliopitiliza na kiwango kikubwa cha cholesterol, ambavyo vyote hivi hupelekea mtu kupata shambulio la moyo kadri muda unavyoenda,” anasema Leah E. Cahill, Ph.D kutoka chuo kikuu cha Harvard.

Pia Cahill ameongeza kuwa kupata kifungua kinywa kunapunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo.

UPI NI MUDA MZURI WA KUPATA KIFUNGUA KINYWA?

Ufuatao ni muda unaofaa kupata kifungua kinywa na vyakula vingine
Kifungua kinywa mda unaofaa ni kuanzia saa moja asubuhi (7am) na saa moja na dakika kumi na moja (7.11am) kama muda sahihi (ideal time)
Chakula cha mchana (Lunch) kuanzia saa sita na nusu mpaka saa saba kamili (12.30pm-1pm)

Chakula cha usiku (dinner) kuanzia saa kumi na mbili kamili mpaka saa moja kamili usiku (6.00pm-7.00pm), kula chakula cha usiku zaidi ya saa moja pia ni hatari kiafya.

Nitoe wito kwa watanzania kwa ujumla kujiatahidi kupata kifungua kinywa kila siku kwa kuchanganya vyakula vyenye protini, wanga, vitamini na madini mbalimbali(minerals). Na pia kujali muda wa kula na kuacha kula chakula kwa mazoea.

Your Health, My Concern

CHANZO: Skipping breakfast may increase coronary heart disease risk.

FORD A. CHISANZA
Intern pharmacist
Tanzania Food And Drug Authority (TFDA)
Location: Off Mandela Road, Mabibo – External,
P.o.Box: 77150, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: [email protected]
[email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents