Burudani

Watu 86,000 wajitokeza kuomba nafasi 600 za kuonekana kama ‘extras’ kwenye Game of Thrones

Mashabiki wa Hispania wa tamthilia ya Game of Thrones walijikuta na furaha kubwa baada ya timu ya utayarishaji kwenda kwenye mji wa Osuna na kutangaza nafasi 600 za kazi.

ad_149580731
Waigizaji wa ziada waliopata kazi wakiwa location

Wengine walikuwa na furaha kubwa kiasi cha kuacha kazi zao zinazoingia fedha nyingi kuhudhuria usahili wa kuonekana kama waigizaji wa ziada (extras) kwenye tamthilia hiyo. Hata hivyo wengine walikosa kwakuwa nafasi zilikuwa 600 pekee lakini watu 86,000 walituma maombi.
ad_149580733

Uchukuaji picha ulianza October 16 na kwa mujibu wa mtandao wa Entertainmentwise, wingi wa maombi ulisababisha server za kampuni ya Fresco Film zilizidiwa nguvu. Maelfu ya watu walimiminika pia kwenye mji huo kwenda kupiga picha na waigizaji wa show hiyo.

zap-game-of-thrones-season-4-pics-014

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents