Picha
Watu 40 wapoteza maisha baada ya lori la mafuta kuwaka moto Kenya
Idadi ya watu waliopoteza maisha baada ya lori la mafuta kugonga magari kadhaa kabla ya kuwaka moto kwenye barabara ya Nairobi-Naivasha nchini Kenya, imeongezeka hadi kufika 40.
Watu wawili walionusurika kwenye ajali hiyo wamelazwa kwenye hospitali ya Nairobi, huku mmoja akiwa amelazwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi.
Mashuhuda waliokuwepo kwenye tukio hilo wamesema dereva wa lori alishindwa kumudu gari lake na kugonga gari jingine na kusababisha magari mengi kugongana. Ajali hiyo iliyotokea kwenye barabara iliyo na shughuli nyingi, kilomita 80 kutoka Nairobi, ilisababisha taharuki kubwa.
Miili mingi kwenye ajali hiyo imeungua kiasi cha kushindwa kutambulika.
Chanzo: Daily Nation Kenya