Promotion

Wateja wa Vodacom waendelea kubadilisha kadi zao za simu kufurahia mtandao wa 4G

Mtandao wenye kasi zaidi wa 4G umekuwa ni habari njema mwezi huu kwa wateja wa Vodacom jijini Dar es Salaam.

4G generic post yassin (2)

Kufuatia kuzinduliwa rasmi, wateja wa Vodacom Tanzania wameendelea kubadilisha kadi zao za simu katika maduka ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam ili kufurahia mtandao wenye kasi ya 4G.
Vodacom Tanzania ilizindua kampeni hiyo Jumatano ya wiki iliyopita inayokwenda kwa kauli mbiu ya HAPA KASI TU yenye lengo la kuwapatia wateja wake huduma ya intaneti yenye kasi zaidi ikijulikana pia kama LTE.

Mbali na kuzindua mtandao wa 4G LTE kampuni hiyo pia imeimarisha mtandao wa 3G ambao unapatikana katika maeneo yote ya miji mikubwa nchini Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia alisema “Huduma hii ni mpya kabisa yenye kasi ya ukweli na kwa kuanzia itatolewa kwa wateja wote wa Vodacom walio jijini Dar es Salaam na kisha itasambazwa mikoani ili kufikia Watanzania wengi zaidi.”

JINSI YA KUBADILISHA KADI YA SIMU KWENDA 4G

Mteja wa Vodacom Tanzania atatakiwa kuwa na simu yenye uwezo wa kupata mtandao wa 4G LTE kisha atatembelea duka la Vodacom lililo karibu naye na atapatiwa kadi ya 4G BURE.

Mbali na kupata kadi hiyo bila malipo mteja pia atazawadiwa kifurushi cha intaneti chenye 4GB BURE. Baada ya kubadilisha sim card yako, fanya speed test kupitia http://speedof.me/ kushuhudia spidi ya hatari na #Vodacom4G #hapakasitu

Unaweza kufahamu zaidi kuhusu mtandao wa 4G na maeneo unapopatikana kwa kubofya HAPA

Tazama video ya msemaji kutoka Vodacom kuhusu 4G

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents