Habari

Watanzania sasa kupata viza ya mwaka mmoja Marekani

WATANZANIA ambao wanasafiri mara kwa mara nchini Marekani sasa watakuwa na nafuu baada ya kurahisishwa kwa taratibu za uombaji wa viza baina ya nchi hizo mbili.

na Mwandishi Wa Tanzania Daima

 

WATANZANIA ambao wanasafiri mara kwa mara nchini Marekani sasa watakuwa na nafuu baada ya kurahisishwa kwa taratibu za uombaji wa viza baina ya nchi hizo mbili.

 

Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini, ilieleza kuwa kuanzia Novemba mosi mwaka huu, ubalozi huo na serikali walizindua taratibu rahisi ya kupata viza.

 

“Ubalozi wa Marekani sasa unatoa kwa Watanzania viza zinazowawezesha kuingia Marekani zaidi ya mara moja ambazo zinadumu kwa mwaka mmoja,” ilisema taarifa hiyo.

 

Awali, viza za nchi hiyo zilikuwa zinadumu kwa muda wa miezi mitatu tu na taarifa ya ubalozi huo ilieleza kuwa chini ya utaratibu wa sasa, muda wa mtu kukaa Marekani utakadiriwa na Ofisa wa Uhamiaji wa Marekani, katika kituo ambacho mgeni ataingilia nchini humo.

 

Aidha, mabadiliko hayo hayahusishi mabadiliko katika gharama za viza ambayo imebakia dola 100 za Marekani. Awali, Watanzania waliokuwa wakihitaji viza za muda mrefu walipaswa kulipia dola 300 za Marekani za ziada.

 

“Watanzania wanaosafiri mara kwa mara kwenda Marekani sasa watapunguza muda na gharama za kuomba na kupata viza. Awali, Mtanzania aliyekuwa anakwenda Marekani mara mbili au tatu, alilazimika kupitia Ubalozi wa Marekani, safari hizo zote na kulipia viza,” ilisema taarifa hiyo.

 

Kwa upande mwingine, rais wa Marekani ambao wanakuja Tanzania, nao watapatiwa viza ya miezi 12 kwa gharama ya dola 100 ambayo itawawezesha kuingia nchini zaidi ya mara moja.

 

Taarifa hiyo ilisema kuwa hatua hiyo imefikiwa kupitia mazungumzo baina ya ubalozi huo na Idara ya Uhamiaji, kupitia kwa Mkurugenzi wake, Kinemo Kihomano.

 

Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, Ubalozi wa Marekani nchini umetoa zaidi ya viza 4,700, kiwango ambacho ni kikubwa katika mwaka mmoja tangu mwaka 2001.

 

Source: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents