Technology

Wataalam waeleza jinsi picha za ‘Selfie’ zinavyoweza kuathiri afya ya akili (mental health)

Kuongezeka kwa joto, madawa ya kulevya na rushwa ni miongoni mwa matatizo yanayoiathiri dunia lakini kwa mujibu wa idara ya afya ya akili ya Thailand, tatizo jingine kubwa linaelekea kuwa tishio kwa maeneo ya nchi – selfie.

selfie2

Jumapili, daktari wa masuala ya akili, Dr. Panpimol Wipulakorn aliwaonya vijana wa Thailand wanaopost picha zao wenyewe kwenye mitandao ya kujamii lakini kushindwa kupata mrejesho chanya (positive feedback) wanakutana na matatizo ya kihisia.

“Kama wakijisikia hawapati likes za kutosha kwa selfie zao kama walivyotarajia, huamua kuweka nyingine, lakini bado hawapati majibu ya mazuri,” alisema.

“Hii inaweza kuathiri namna wanavyofikiri. Wanaweza kupoteza kujiamini na kuwa na mtazamo hasi kwa wao wenyewe kama vile kujihisi wana kasoro.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents