Habari

Wasomi wengi hawawezi kufanya biashara, ila wanasaidia biashara nyingi kukua

Unapotazama kwa umakini suala la uchumi na mambo ya biashara utagundua wamiliki wakubwa wa biashara nyingi sio wasomi sana ukilinganisha na walioajiriwa kuendesha hizo biashara.

SA-image-business-woman-2

Nilipokuwa nikisoma maelezo ya mtu mmoja alizungumzia kitu fulani cha msingi ambacho kinatukabiri sisi ambao kwa namna moja ama nyingine tunasema ni wasomi lakini hatuwezi kuendesha biashara zetu wenyewe. Kitu unachotakiwa kujiuliza kwanini siwezi kufanya biashara kama nimesoma kweli ila namweza kuwa meneja mauzo wa kampuni fulani na kufanikiwa kwenye kitengo hicho?

Je inamaanisha elimu tulizonazo hazina uwezo wa kutusaidia mpaka tuajiriwe tu? Hapa nazungumzia watu tuliosoma biashara, uongozi wa biashara na ujasiriamali na vitu vingi ambavyo tumepewa kwenye vyeti vyetu kwamba tulifaulu. Hebu fuatilia nini kinatusumbua;

Wasomi wengi tunajua vitu kwa maandishi lakini sio kwa kutenda. Ni kweli umekwenda shule au madarasa ya kutosha unaweza kuandika mchanganuo mpaka watu wakashangaa, tatizo ni kwamba hatuna uwezo wa kuanzisha kitu kidogo kikaendana na elimu yetu tuliyonayo. Tunafanya sana uchunguzi na kuangalia endapo biashara itafanikiwa tunaishia kuogopa na kutofanya kabisa.

Wasomi wengi hawana uthubutu katika maamuzi ya kuanzisha kitu chochote. Kama ilivyo kwa mtu mwingine yeyote inapokuwa ni kazi ngumu kufanya maamuzi ambapo unaona kabisa kuna mbadala ambao ni rahisi kuuchukua. Wengi wanaona ni afadhali kuajiriwa na kupata mshahara hata kama sio kile ambacho walitarajia ila angalau kinakidhi mahitaji na maisha yanakwenda mbele. Kwa lugha nyepesi ni waoga sana , wengi wanaogopa endapo biashara ikigoma ni nini matokeo yake? wataishije? na maisha yao ya baadaye yatakuwaje?

Wasomi wengi wanaangalia wanachopata sasa na si cha baadaye. Kama kila mtu angeweza kujua faida ya kitu anachofanya sasa au kuwekeza sana kitakuwaje hapo baadaye ingekuwa rahisi sana kila mtu kufanya biashara au kuwa na mradi wake binafsi. Ingawa tumelalamikia mazingira mabaya ya uchumi na uongozi bali sisi wenyewe taujaweza kuthubutu kufanya kitu hata kidogo ambacho wengine ambao hawajabahatika kusoma waweze kujifunza kitu cha tofauti.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents