Burudani

Washindi wa tuzo za Grammy hupewa fedha? Ukweli huu hapa

Watu wengi wamewahi kujiuliza iwapo washindi wa tuzo za Grammy, tuzo zenye heshima zaidi nchini Marekani, hupewa pia fedha.

Kwenye tuzo za Grammy mwaka huu Adele aliibuka na ushindi mzito ukiwemo wa album ya mwaka, 25

Mtandao wa BlackEnterprise.com ulifanya uchunguzi kutafuta majibu na kubaini kuwa si tu washindi hawapewi hata senti moja, bali hata wale wanaotumbuiza pia, hawalipwi chochote. Hata hivyo tuzo wanazopewa ambazo hutengeneza kwa dhahabu huwa na thamani kubwa.

Hata hivyo kuna faida kubwa ambayo huja baadaye kwa washindi. Mtandao wa Forbes umewahi kuripoti kuwa wasanii wanaotumbuiza huongeza asilimia 55% ya mauzo ya tiketi kwenye show zao. Watayarishaji wa muziki nao hunufaika vile vile.

Watayarishaji wa muziki wanaposhinda tuzo za Grammy huweza kuongeza bei katika kazi wanazofanya. Watayarishaji wa muziki ambao hawajashinda tuzo za Grammy hutoza wastani wa $30,000 hadi $50,000 kwa wimbo mmoja. Wakishinda tuzo hiyo gharama ya kuanzia hupanda hadi kuwa $75,000 na watayarishaji wakubwa zaidi huweza kutoza mara mbili ya hiyo.

Pamoja na kutumbuiza, Beyonce ni mmoja ya waimbaji walioshinda Grammy mwaka huu

Kushinda Grammy hubadilisha namna msanii anavyochukuliwa. Kwa mfano, baada ya Bruno Mars kushinda, gharama za show kwa siku ilipanda kutoka $130,000 hadi $202,000 (+55%) huku Taylor Swift akitoka $125,000 hadi $600,000 (+380%).

Chance The Rapper amewashangaza wengi mwaka huu kwa kushinda tuzo za 3 za Grammy bila kuwa chini ya label yoyote na muziki wake huutoa bure mtandaoni. Thamani yake inatarajiwa kupanda kwa kiasi kikubwa baada ya ushindi huo

Pia wageni wanaolikwa kwenye tuzo hizo, hawaondoki mikono mitupu. Hutoka wakiwa na mifuko ya zawadi zenye thamani zaidi ya mishahara ya watu. Mwaka 2010 zawadi zilizokuwa kwenye mifuko iliripotiwa kuwa na thamani ya $50,000.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents