Burudani

Wasanii wengi wa sasa watapotea, wanatunga nyimbo zenye ladha ya ‘bubble gum’ – Squeezer

Msanii wa muziki ambaye zamani aliwahi kufanya vizuri wimbo Bachelor, Squeezer amefunguka juu ya muziki unaofanywa na vijana wengi wa sasa kwamba hauwezi kudumu kwani wengi wanaokimbilia kufanya sanaa hiyo hawana ubunifu wa kutosha.

Muimbaji huyo amedai nyimbo nyingi za vijana wa sasa zikisikilizwa mara kwa mara zinakera masikio ya watu.

“Nyimbo pamoja na wasanii wengi wa sasa wapo mbioni kupotea kutokana na kuwa na ubunifu mdogo sana katika kazi zao, wengi hawana ‘knowledge’ ya kutosha. Wanatunga nyimbo zenye ladha ya ‘bubble gum’ mtaani wanaziita hivyo kwa kuwa haziwezi kudumu zaidi ya miezi miwili. na nyie watangazaji mnavyozipa muda hewani ndo zinakuwa hata mwezi haziwezi kusurvive”. Squeezer alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.

Msanii huyo ameongeza kwa kuwashauri wasanii warudi shule ili kupata uelewa katika kuboresha kazi zao na kusisitiza kwamba kama ni muziki upo kila siku na siku zinavyozidi kwenda hela zinazidi kuwa nyingi na kunamuongezea heshima msanii.

Pia muimbaji huyo aliyewahi kutamba na ngoma iitwayo ‘Naja’ aliyomshirikisha Juma Nature amesema huo ndiyo wimbo uliompatia mashabiki wengi ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na mafanikio mengi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents