Burudani

Wasanii wachanga msisubirie kusaidiwa, watu wana roho mbaya – Gabo

Msanii wa filamu ambaye anakuja kwa kasi nchini, Salim Ahmed aka Gabo Zigamba amewataka wasanii wachanga wa filamu kuacha kusubiria kusaidiwa na watu.
gabo

Muigizaji huyo ambaye ni mmoja kati ya wasanii wanaowania Tuzo za EATV Award 2016, amedai wapo watu ambao wanajitokeza kutaka kusaidia wasanii wachanga kumbe wanania ya kuwanyonya.

“Watu wana umoja wa mdomoni lakini mioyoni hawapo hivyo, tuna umoja wakuusema lakini sio moyoni. Kila mmoja anataka kufanya kitu peke yake, kwa hiyo watu wana roho mbaya. Mimi ni akili yangu ndio kitu ambacho kimenifanya nifike hapa, watu wanataka kukusaidia lakini kumbe wanataka wakutumie tu,” alisema Gabo.

Pia Gabo alisema wasanii wakijitambua na kutambua thamani yao wataweza kufika mbali bila kutegemea watu wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents